Soma habari Hii ....Ujue Rais Mstaafu JK Kafanya ‘nini’ ughaibuni

Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania
Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete, amekataa kuzungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani huku msaidizi wake akiwapiga vikumbo waandishi hao ili wasimsumbue ‘bosi’ wake, baada ya kutoka katika mkutano wa 71 wa Umoja wa Mataifa, anaandika Charles William.
Mkutano huo ulioanza jana mjini New York, unajadili masuala mbalimbali ikiwemo vita dhidi ya ugaidi pamoja na utolewaji wa misaada zaidi kwa wakimbizi.
Mkanda wa video uliopatikana leo, umemuonyesha Rais Kikwete akitoka katika eneo la mkutano huku wandishi wa habari wakijaribu kumuhoji lakini akikataa na kuendelea kutembea, akiondoka katika eneo hilo.
Baada ya Rais Kikwete kukataa kuhojiwa alionekana akiwatupia maneno waandishi hao. Hata hivyo maneno hayo hayakuweza kunaswa na vinasa sauti vya wandishi hao huku msaidizi wake akiwazuia waandishi hao ili wasiendelee kumsogelea.
Haikujulikana mara moja, kwanini Rais Kikwete alikataa kuzungumza na wandishi wa habari katika eneo la nje ya mkutano huo, ikizingatiwa kwamba katika siku za nyuma amekuwa ‘rafiki’ kwa waandishi.
Si Rais Kikwete pekee ‘aliyewachomolea’ waandishi wa habari, isipokuwa hata Christine Lagarde, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya fedha ya kimataifa (IMF), naye hakuwa tayari kuzungumza na wanahabari baada ya kutoka katika mkutano huo.
Mkutano huo wa 71 wa UN umeendelea tena leo ambapo Rais Barrack Obama wa Marekani, amehutubia akizungumzia suala la kuongeza misaada kwa wakimbizi ikiwemo utolewaji wa elimu kwa wakimbizi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment