Pichani wa pili kutoka kushoto mwenye suti nyeusi ni DC. Mhando akiwahoji wavamizi wa Ardhi ya wananchi wa Kijiji cha Kabage.
…………………………………………………..
Na Ezron Mahanga,Katavi.
Takribani Hekali 501 zimerudishwa
mikononi mwa wananchi wa kijiji cha Kabange kata ya Sibwesa wilaya mpya
ya Tanganyika mkoani Katavi baada ya kushikiliwa na wavamizi wa kikundi
cha Nguvu kazi Group kwa miaka 9 sasa waliolivamia eneo la bonde la
kijiji hicho kwa kutumia nyaraka za kugushi na kulitumia eneo hilo kwa
ajili ya kilimo cha zao la mpunga
Hayo yamebainishwa na mkuu wa
wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando kwenye kikao cha ndani
kilichofanyika katika shule ya msingi Kabage mara baada ya kutembelea
eneo hilo lenye mgogoro kwa miaka 9 hali iliyopelekea vifo vya wananchi
zaidi ya 6 katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita kwa ajili ya
kugombania Ardhi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi
waliohudhuria katika kikao hicho wameipongeza Serikali kwa kutatua
mgogoro huo huku wakieleza kuwa waliishi pasipo kuwa na amani kwa
kuhofia maisha yao.
Aidha kwa Upande wake Afisa Ardhi
wa wilaya ya Tanganyika Bwana Mussa Yohana amewataka wananchi kufuata
sheria za kumiliki Ardhi kihalali ili kuepusha migogoro ambayo imekuwa
kero katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo.
Nae katibu wa kikundi cha Nguvu
kazi group Ramadhani Kasonso akiongea mbele ya wananchi wa kijiji hicho
mara baada ya kuamriwa kurudisha Ardhi kwa wanakijijii amewaomba kusahau
yaliyopita na kuendeleza ujenzi wa taifa huku akiomba uongozi wa kijiji
hicho kulipa Trekta ya kulimia mali ya Nguvu kazi Group ambayo
ilichomwa moto na wananchi kutokana na mgogoro huo.


0 comments :
Post a Comment