WAZIRI MKUU MAJALIWA KUHAMIA DODOMA LEO


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuhamia rasmi leo mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Julai 25, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imeandaa mapokezi ya Waziri Mkuu atakapowasili mchana na kuanzia kesho atafanya ziara ya siku mbili katika manispaa ya Dodoma kukagua hatua za maandalizi ya kupokea ujio wa Serikali.

Taarifa ya ofisi ya mkoa imesema Majaliwa atatembelea maeneo ya kutolea huduma za afya, kituo cha umeme cha Zuzu, masoko, chanzo cha maji cha Mzakwe na maeneo ya viwanda.

Ofisa habari wa mkoa, Jeremiah Mwakyoma amesema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mapokezi hayo yamekamilika.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment