Kiongozi
wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe amesema Tanzania haina
dikteta uchwara na kudai kuwa ina dikteta mambo leo.
Zitto
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya msemaji wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Ole Sendeka kusema kuwa nchi haiendeshwi kidekta na
kwamba wanaosema hivyo ni wachache waliobanwa kutafuna mali na fedha za
nchi.
Zitto amefafanua kuwa dikteta uchwara ni kiashiria cha udikteta na kwamba nchi haina kiongozi wa aina hiyo.
Ameeleza kuwa dikteta mambo leo ni kiongozi anayetaka kutatua kero za wananchi pasipo kutaka kuhojiwa.
“Dikteta
mambo leo anawapa mnachotaka ila msihoji vinapatikanaje. Tabia hiyo ipo
hapa nchini mfano serikali imenunua ndege pasipo kutaja gharama za
manunuzi, inawezekanaje ikawa siri wakati fedha zilizotumika ni kodi za
wananchi na si mtu binafsi? “
Ameongeza kuwa “Pia hatuna dikteta kwa sababu siamini kama rais na kundi lake litajinufaisha na mali za watanzania, “
Hata
hivyo, Zitto amewaasa viongozi wa upinzani walioshikilia halmashauri za
manispaa na miji, kuzifanya manispaa zao kuwa mfano wa kuigwa katika
maendeleo na utatuaji wa kero za wananchi badala ya kuilalamikia
serikali kuwa haitatui kero za wananchi wake.
“Karibu
manispaa 35 zinashikiliwa na upinzani ambao umepewa dhamana na wananchi
kuwaletea maendeleo na kwamba wasipo tekeleza ahadi zao hakuna
wakumlaumu kwa sababu Rais John Magufuli hawezi sambazia watu huduma za
maji, dawa na kadhalika,” amesema.
Vile vile ameshangazwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuingilia majukumu ya Meya wa jiji hilo
“Mkuu
wa mkoa anatenda majukumu ya meya kivipi? Hana mamlaka hayo,wenye
jukumu la kusimamia usafi ni manispaa ikiongozwa na meya yeye anaingilia
kwa nini? ” amehoji Zitto.


0 comments :
Post a Comment