Kuelekea
mchezo wa EPL kati ya Liverpool na Machester United unaotaraji kupigwa
Jumatatu usiku, kocha wa Man United, Mreno Jose Mourinho amezungumza
kuhusu mchezo huo na kusema kuwa amejipanga kwenda kufanya kazi yake
ambayo aliajiriwa kuifanya.
Mourinho
amesema mara kadhaa amecheza katika uwanja wa Liverpool, Anfield akiwa
na timu ya Chelsea hivyo hakuwa akifahamu ukubwa wa mchezo wa Man United
na Liverpool na sasa anafahamu hivyo amejipanga kwa ajili ya mchezo
huo.
“Sijawahi
kucheza hii mechi, lakini nimecheza mara nyingi dhidi ya Liverpool,
mara nyingi dhidi ya Manchester United, nafahamu ukubwa wa hizi klabu,
na sasa naelewa vizuri ukubwa wa kihistoria ya hawa wapinzani wakubwa
wawili. Nitakwenda kucheza mchezo wangu. Nitaenda kufanya kazi yangu na
kawaida ninafurahia kazi yangu,
“Napenda
hali ya mchezo, ni sifa ya hizi mechi, lakini kuwa meneja wa Manchester
United inamaana zaidi, kwasababu hatuwezi kulinganisha historia kati ya
timu yangu iliyopita [Chelsea] na United na Liverpool,” alisema
Mourinho na kuongeza.
“Naangalia
mbele kwa ajili ya hilo. Napenda kucheza Anfield. Nimeshinda mara
nyingi pale pia nilipoteza. Nimeshinda mechi kubwa na nimepoteza mechi
kubwa, kwahiyo siwezi kusema napenda kwenda sababu nilifanikiwa, sababu
sio kweli, lakini napenda kwenda pale [Anfield],” alisema Mourinho

0 comments :
Post a Comment