Mchezo wa VPL kati ya Simba iliyokuwa mwenyeji wa Kagera Sugar umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila.
Magoli
ya Simba yamefungwa na beki Mzarimu Yassin akiunganisha mpira wa kona
uliopigwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 44 na goli la pili
likifungwa na Shiza Kichuya kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 75.
Ushindi
huo unaiwezesha Simba kufikisha alama 23 katika michezo tisa
iliyocheza, ikishinda michezo saba na kutoa sare miwili na ikiwa na
mchezo mmoja mkononi, Kagera Sugar inasalia kuwa na alama 15 ikiwa
katika nafasi ya tatu ya msimamo wa VPL.


0 comments :
Post a Comment