![]() |
| FRIENDS RANGERS |
Ligi
hiyo ya Daraja la Kwanza itaendelea Jumapili Oktoba 9, 2016 kwa mchezo
utakaozikutanisha Ashanti United na Friends Rangers; zote za Dar es
Salaam. Kadhalika Jumatatu, kutakuwa na mchezo kati ya Mshikamano ya Dar
es Salaam na Lipuli ya Iringa. Mchezo huo, pia utafanyika Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.
Kundi
B; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Kurugenzi ya
Iringa na Coastal Union ya Tanga ufakaofanyika huko Mufindi ukifuatiwa
na michezo mitatu siku ya Jumapili Oktoba 9 ambayo Mlale itacheza na
Majimaji ya Songea huko Uwanja wa Majimaji Njombe Mji itaikaribisha
Kemondo wakati KMC itacheza na Mbeya Warriors kwenye Uwanja wa Mabatini,
Pwani.
Kundi
C; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu Mvuvumwa ya Kigoma itacheza na Stand
United ya Singida wakati Panamo itapambana na Alliance huku Polisi
Dodoma itacheza na Polisi Mara wakati Jumapili Rhino ya Tabora itakuwa
mwenyeji wa Mgambo JKT ya Tanga.



0 comments :
Post a Comment