| MASHABIKI WA MBEYA CITY |
Ligi
Kuu ya Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Oktoba 7, 2016
kwa michezo miwili ambako Kagera Sugar itaikaribisha Toto Africans
kwenye Uwanja Kaitaba mkoani Kagera wakati Stand United itakuwa mgeni wa
Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mbali
ya mechi hizo za kesho, Jumamosi Oktoba 8, 2016 pia kutakuwa na michezo
mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itaikaribisha
Ndanda FC jijini Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikiialika Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.
Kwa
upande wa Ligi Daraja la Kwanza, kundi A Jumamosi Oktoba 8, kutakuwa na
mchezo kati ya Pamba ya Mwanza na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Karume,
Ilala jijini Dar es Salaam es Salaam wakati African Sports itakuwa
mwenyeji wa Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


0 comments :
Post a Comment