Shirikisho
la Soka Duniani (FIFA) limetangaza majina ya wachezaji 30 ambao
wanataraji kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia kwa mwaka 2016 maarufu
kama Ballon d’Or.
Majina
ya wachezaji ambao wanawania tuzo hiyo kwa mwaka huu imeongezeka kutoka
23 hadi 30 na Disemba, 13 yatatangazwa majina ya wachezaji watatu ambao
wataingia katika kinyang’anyiro kwa kupigiwa kura na mshindi
kupatikana.
Wachezaji
30 ambao wametajwa kuwania Ballon d’Or 2016 ni, Sergio Aguero
(Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth
Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo
(Real Madrid), Kevin De Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala
(Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico
Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Manchester
United), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Toni Kroos
(Real Madrid), Robert Lewandowski (Bayern Munich).


0 comments :
Post a Comment