LOWASSA AMKUMBUKA MWL NYERERE KWA TUKIO LA MWAKA 1991..!!!


Moja ya Jambo ambalo nimeona ni vema nikamkumbuka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere siku ya leo Oktoba, 14 ni uwezo wake wa kuona mbali hasa pale aliposhauri Uanzishwaji wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa mwaka 1991 baada ya Tume ya Jaji Nyalali kuwasilisha maoni yake kwa Rais Mwinyi.


Taifa letu linahitaji aina ya viongozi wenye uwezo wa kuona mbali zaidi, kuona kabla ya wengine na kuona sana kuliko wengine. Tangu awamu ya kwanza mpaka leo Taifa letu bado halijapata kiongozi mfano wa Nyerere katika kuona mbali, bado hatujapata!

Uongozi ni kuona mbali kuliko wengine. Pamoja na kuwa asilimia 80 ya waliohojiwa na Tume ya Jaji Nyalali hawakutaka mfumo wa vyama vingi vya siasa na asilimia 20 pekee ndio waliotaka, bado uamuzi ulifanyika kwa kuzingatia vision ya Mwalimu Nyerere kuwa Taifa letu sasa ni wakati muafaka tukaenda na Mfumo wa vyama vingi vya Siasa.

Leo hii, kila anayejigamba kumuenzi Mwalimu Nyerere na maneno yake na vitendo vyake vinaashiria ama kuzuia au kuminya Uhuru wa vyama vingi ni muongo na wala hawezi kutuminisha kuwa anamuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuwa vitendo na maneno yake vikakinzana na dira aliyotuachia Mwalimu Nyerere.

Tunaowajibu sisi kama viongozi kuzitafakari njia zetu ili kujenga msingi imara wa maendeleo ya Taifa letu. Taifa letu kwanza, mengine baadaye kwa kuwa Taifa letu ni kuu na kubwa kuliko matamanio yetu ya kuwa viongozi na kuzidi yote Taifa letu ni kuu kuzidi rangi ya bendera za vyama vyetu.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment