UONGOZI wa klabu ya Simba leo unatarajia kuwasilisha rasmi malalamiko
yake kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (TLB) ili
imchukulie hatua mwamuzi wa mechi yao dhidi ya Yanga, Martin Saanya.
Simba na Yanga zilikutana kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki na
kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi hiyo iliyojaa vurugu.
Vurugu hizo zilitokana na bao la kuongoza la Yanga lililofungwa na
Amisi Tambwe ambalo lililalamikiwa kwani kabla hajafunga, mchezaji huyo
alishika mpira kwa mkono jambo lililozua vurugu kwa mashabiki wa Simba
kwani mapema Ibrahim Ajibu aliifungia Simba bao lililokataliwa na
mwamuzi kwa madai alikuwa ameotea.
Mashabiki hao walikwenda mbali kwa kung’oa viti vya uwanja huo na kuvirusha uwanjani.
“Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba imesikitishwa sana na vitendo
vilivyofanywa na baadhi ya mashabiki wetu vya kuvunja sehemu ya viti vya
Uwanja wa Taifa, kitendo kilichotokea jana (juzi) kwenye mchezo wetu wa
Ligi Kuu dhidi ya Timu ya Yanga…
“Sisi tunaamini vitendo viovu vilivyofanywa na mashabiki wetu
vilisababishwa na uamuzi wa hovyo kupita kiasi uliosababishwa na waamuzi
hao hasa Martin Saanya,” alisema Manara.
“Haieleweki ni kigezo gani mwamuzi huyo alitumia kulikubali goli la
'mpira wa pete'la mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe na kulikataa goli
halali la mshambuliaji wetu Ibrahim Ajibu.
Katika mchezo huo vurugu
kubwa zilizozuka na kusababisha askari kutumia nguvu ya ziada kwa
kutumia mabomu kutuliza vurugu hizo ambazo baadhi ya watu waliumia
vibaya.



0 comments :
Post a Comment