MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ameonesha kusikitishwa na sintofahamu inayoendelea kuhusu uhamisho wa kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Farid Mussa kwenda Hispania kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya Teneriffe.
Samatta ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars, ameandika kwenye
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kusema aliposikia
Farid anaenda Hispania kwa majaribio alipata furaha kwa kuamini kwa
kipaji chake asingeshindwa kufuzu na furaha yake iliongezeka baada ya
kusikia amefuzu.
Pia Samatta aliendela kuandika kuwa alikuwa na furaha kwa sababu
aliamini maendeleo ya timu ya taifa yatapiga hatua haraka ikiwa na
wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.
“Kadri siku zinavyokwenda nimekuwa simsikii Farid kwenye klabu yake
ya Teneriffe na habari zilizopo bado yupo Tanzania, Je ni kwa nini bado
yupo Tanzania wakati kila kitu kilishakwisha na ni nani mwenye jibu la
hili, tahadhari, kuna nini nyuma ya pazia?” Alihoji Samatta.



0 comments :
Post a Comment