
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.

Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa Kwanza wa wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Morocco Makamu wa Rais aliainisha maeneo mbali mbali ambayo yanaweza kuwa fursa nzuri ya kuwekeza Tanzania.
Baadhi ya maeneo hayo ni Kilimo,Utalii, Nishati, Mafuta na Gesi, Viwanda,Sekta ya Huduma, na Sekta ya Madini. Mbali na kuainisha baadhi ya fursa Makamu wa Rais aliwahakikishia uwepo wa amani na usalama na sheria mbalimbali zinazolinda haki za wawekezaji.

Rais wa
Chama cha Wafanyabiashara wa Morocco Bi.Miriem Bensalah-Chaqroun,
akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Biashara na Uwekezaji baina ya
Tanzania na Morocco uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.

Waziri
wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati
wa mkutano wa kwanza uliowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na
Morroco.

Sehemu ya wafanyabiashara kutoka Morocco wakifuatilia kwa makini mkutano huo


0 comments :
Post a Comment