Kikosi
cha Kupambana na wezi wa magari cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa makosa ya wizi
wa magari.
Kamishna
wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
amesema kikosi hicho pia kimefanikiwa kukamata mtandao huo pamoja na
kukomboa magari manne yaliyoibwa na watuhumiwa hao.
Amesema
miongoni mwa watuhumiwa hao ni mwanafunzi wa chuo cha CBE aliyemtaja
kwa jina la Dikson Valentino Godfrey (23) ambaye makazi yake ni Kimara.
Amewataja wengine kuwa ni Denis Ushaki(25), Alfred Ditriki(33) Venance Bureta(24).
Katika
tukio lingine, Kamanda Sirro ameeleza kuwa, askari polisi walifanikiwa
kukamata magari matatu ya wizi yaliyoibwa Dar es Salaam na kufichwa
mkoani Arusha.
Amesema
watuhumiwa wa mtandao huo wanashikiliwa Arusha na kwamba juhud za
kuwafuata zinafanyika ili kujibu mashtaka yanayowakabili.
Hata
hivyo, Kamanda Sirro amesema jeshi la polisi limekamata watuhumiwa 57
kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuvunja nyumba usiku na kuiba, kuvuta na
kuuza bangi, kunywa na kuuza gongo pamoja na vikundi vya panya road.


0 comments :
Post a Comment