Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU
ya Fanja ya Oman, imefanikiwa kupata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa
(ITC) ya kiungo mkongwe kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa na
sasa inaweza kuanza kumtumia katika Ligi ya nchi hiyo na Ligi ya
Mabingwa Asia.
Akizungumza
jana kutoka Oman, Ngassa alisema kwamba ITC yake imefika na Ijumaa
alichezamechi yakeya kwanza wakifungwa 3-0 ugenini na Dhofar Uwanja wa
Youth Complex mjini Salalah.
Ngassa amejiunga na Fanja kwa mkataba wa miaka miwili akitokea ya Free State Stars ya Afrika Kusini.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba,
Yanga SC, Azam FC na Simba za Dar es Salaam anajiunga na wawakilishi hao
wa Oman kwenye Ligi ya Mabingwa ya Asia, aliondoka Free State mwezi
uliopita baada ya kuomba mwenyewqe kuvunja Mkataba.
Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka jana akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri kwa mkataba wa miaka minne.
Hata
hivyo, kocha aliyemsajili baba huyo wa Farida (9) na Faria (7)
alifukuzwa baada ya miezi miwili tu na sasa tayari yuko Mbeya City ya
Tanzania.
Katika
kipindi cha mwaka mmoja wa kuwa Free State, Ngassa alifanya kazi na
makocha wanne akiwemo huyu wa sasa, Mfaransa Denis Lavagne aliyeanza
kazi Juni mwaka huu.
Wengine
ni Mjerumani Ernst Middendorp aliyefanya kazi kati ya Septemba na
Desemba 2015, Mtaliano Giovanni Solinas aliyefanya kazi kati ya Desemba
na Mei 2016.
![]() |
| Ngassa sasa ameanza kucheza Ligi ya Oman |



0 comments :
Post a Comment