Jana October 6 2016 imeripotiwa habari ikitokea eneo la Katarabuga, kata ya
Bwanjai wilaya ya Misenyi Kagera ambapo wananchi wa bonde la Katarabuga
wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka moto ardhini wakidhani volcano.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Prof. Abdulkarim
Mruma amesema moto huo ni wa kawaida tu hivyo wananchi wasiwe na
taharuki yoyote.
Prof.
Mruma akitoa ufafanuzi juu ya uvumi huo amesema moto huo ni wa kawaida
na kwamba unatokea kwenye ardhi ambayo ina uozo wa majani mengi na yale
majani yakiungua yanatoa kitu kama hicho. Prof.
Mruma ameongeza kuwa moto wa namna hii mara nyingi unatokea kwenye
makaa ya mawe mtu anapita anaangusha moto mkaa unalipuka panaanza
kuungua na ardhi inachubukachubuka kama ilivyotokea kwenye ebneo hilo.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)


0 comments :
Post a Comment