Michezo
mitano ya kutafuta nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia 2018 kwa nchi za
America Kusini imechezwa, mmoja wapo ukiwa ni mchezo wa Brazil
iliyokuwa mwenyeji wa Bolivia, Brazil ikiibuka na ushindi wa goli 5-0.
Magoli
ya Brazil katika mchezo huo yalifungwa na Neymar dk. 11, Phillip
Coutinho dk. 26, Filipe Luis dk. 39, Gabriel Jesus dk. 44 na Robert
Firmino katika dakika ya 76.
Aidha
katika mchezo huo, staa wa Brazil, Neymar alilazimika kutoka dakika ya
68 na kumpisha William baada ya kupigwa kiwiko na beki wa Bolivia,
Ronaldo Raldes na kusababisha kupasuka usoni.
MO Blog imekuandalia picha za jinsi tukio hivyo lilivyojitokeza.


0 comments :
Post a Comment