Licha kuisaidia Real Madrid kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) mwaka huu, hilo halijawa sababu kwa staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo jina lake kutajwa kuwa tatizo klabuni hapo.
Hilo limeelezwa na kocha wa zamani wa Real Madrid, Fabio Capello kuwa tangu kuanza kwa msimu wa 2016/2017, Ronaldo amekuwa katika kiwango kibovu ambacho kinaweza kuigharimu timu na kufanya vibaya katika michezo yake.
Alisema yawezekana hali hiyo kwa Ronaldo inajitokeza kutokana na majeruhi aliyoyapata katika mchezo wa fainali ya Europa wakati Ureno ilipopambana na Ufaransa, hivyo ni vyema mchezaji huyo akapata muda wa kupumzika ili kurudi katika ubora wake.
“Tatizo sasa Real Madrid ni Cristiano Ronaldo,” alisema na kuongeza”Sababu hayupo katika kiwango kizuri na ndiyo mchezaji wao bora”