Mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba iliyyokuwa mwenyeji wa Toto
Africans ya Mwanza umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli tatu
kwa bila.
Ushindi
wa Simba umepatikana kupitia Mzamiru Yassin akifunga magoli katika
dakika ya 42 na 74, na goli lingine likifungwa na mchezaji raia wa
Burundi, Laudit Mavugo katika dakika ya 51.
Kwa
matokeo hayo Simba imefikisha alama 29 ikiongoza msimamo wa VPL,
imecheza michezo 11 na ikiwa na mchezo mmoja mkononi, nafasi ya pili
ikishikiliwa na Yanga yenye alama 21 huku Toto Africans ikisalia mkiani
na alama nane katika michezo 12.
Mchezo unaofuatia kwa Simba ni Jumamosi ya Oktoba, 29 dhidi ya Mwadui ya Shinyanga.


0 comments :
Post a Comment