Staa wa Chelsea kafiwa na mama yake mzazi


Winga wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya Chelsea ya England Willian amepata pigo baada ya kupokea taarifa za kumpoteza mama yake mzazi Maria Jose, Willian amepokea taarifa za kumpoteza mama yake aliyekuwa ansumbuliwa na kansa.
Maria Jose alifariki kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa kipindi cha miaka miwili, Maria amefariki akiwa hospital Sao Paulo Brazil, kufuatia taarifa hizo Willian ataukosa mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Leicester City weekend hii, Chelsea imeoneshwa kuguswa na msiba wa mama wa mchezaji wao na kutuma ujumbe wa rambirambi.
jibapa
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Willian alijiunga na Chelsea mwaka 2013 akitokea Anzhi Makhachkala ya Urusi aliyokuwa kadumu nayo kwa kipindi kifupi akiichezea mechi 11, Willian pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichoifunga Venezuela goli 2-0 siku ya  Jumanne.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment