Miongoni
mwa mchezo mkali jioni ya leo ni ule utakaowakutanisha Wanajangwani
Yanga dhidi ya Wanarambaramba Azam FC mchezo utakaopigwa Jijini Dar es
Salaam. Timu hizo zinashuka dimbani huku zikiwa na kumbukumbu mbaya ya
kupoteza mchezo mmoja mmoja kwa kila timu baada ya kukubali kichapo
kutoka kwa Stendi United ya Mkoani Shinyanga hivyo leo kila mmoja
atashuka dimbani kujaribu kusawazisha makosa ya kupoteza mchezo huo.
Timu
za Azam na Young Africans; zote za Dar es Salaam huku mwamuziki wa
mchezo huo Na. 76 atakuwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo
atasaidiwa na Soud Lila na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen
Mduma; wote wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael
Wambura pia wa Dar es Salaam.
Mchezo
Na. 77 utazikutanisha timu za Ruvu Shooting na Mbeya City, kwenye
Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Rudovic
Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jeremina
Simon wa Dar es Salaam. Kamisha wa mchezo huo atakuwa Idelfonce Magali
wa Morogoro.
Mtibwa
Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza kwenye
Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. Mchezo huo Na. 78 utachezeshwa na
Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi ni Ferdinand Chacha wa
Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa akiba Nicolaus
Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa Dodoma.
Mchezo
mwingine utakuwa ni kati ya Toto African ya Majimaji ya Songea kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mchezo huo Na. 79 utachezeshwa na mwamuzi
Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius
Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa
Mwanza. Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar es Salaam.


0 comments :
Post a Comment