Hazard kasema anaweza kuhama Chelsea ila baada ya kufanya hivi


Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji anayeichezea Chelsea ya London Eden Hazard November 18 2016 alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi October, baada ya kucheza mechi nne, kufunga goli tatu na kutoa assist katika ushindi wa Chelsea wa mechi zote nne.
Eden Hazard ambaye amekuwa akitajwa kuhitajika kwa miaka kadhaa sasa na klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa na kuwa amekuwa akisisitiza kuwa na furaha katika klabu ya Chelsea, ameweka wazi kuwa anaweza kuondoka Chelsea ila ni baada ya kutwaa Ubingwa.
“Ndio naweza kuondoka Chelsea siku moja lakini ni baada ya kuisaidia kutwaa Ubingwa, unahitaji kucheza vizuri na kwa kujitoa ili watu waweze kukukumbuka kwa sababu za msingi”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment