Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Sevilla ya Hispania kwa mkopo akitokea Man City Samir Nasri siku kadhaa nyuma alisikika akisema ocha wa Man City Pep Guardiola aliwakataza wachezaji wasifanye mapenzi baada ya saa sita usiku ili wapate muda wa kutosha kupumzika.
Stori kutoka BBC Sport akinukuliwa kocha wa Man City Pep Guardiola akizungumzia
ishu hiyo, ameeleza kuwa hajawahi kukataza wachezaji kufanya mapenzi na
wapenzi wao na anaamini kuwa mchezaji akifanya mapenzi ndio anacheza
vizuri.
Nasri na Pep Guardiola
“Haiwezekani
kuwa mchezaji mzuri kama hufanyi mapenzi na mpenzi wako, sijawahi
kukataza wachezaji wasifanye mapenzi na sitakataza kama utakuwa ukifanya
hivyo wewe ni mchezaji mzuri” >>> Guardiola
Hata hivyo Pep Guardiola amewahi kuripotiwa kuweka sheria kadhaa katika kikosi chake cha Man City ili kujenga timu yenye mshikamano, Guardiola anaripotiwa kupiga marufuku huduma za Wi-fi katika maeneo ya uwanja wa mazoezi ya Man City.


0 comments :
Post a Comment