Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wengine watatu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa wenyeviti wawili wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii na mmoja wa chuo.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi iliwataja walioteuliwa kuwa ni kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Alhaji Mussa Iyombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Mhandisi Alhaji Mussa Iyombe ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Pili, Rais Magufuli amemteua Prof. Faustine Karani Bee kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF)

Prof. Faustine Karani Bee ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Tadeo Andrew Satta kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Kabla ya uteuzi huu Prof. Tadeo Andrew Satta alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment