
1. Ni watu wenye tabia ya kujipendelea wao wenyewe, watu wenye umimi na ubinafsi wakati wote.
2.
Ni watu wenye tabia ya ubishi na kupinga kila jambo, hususani lile
ambalo mwingine amelisema ama kulizungumza, kwao hoja ya mwingine sio
hoja bali hoja yao ndiyo hoja pekee.
3.
Ni watu wenye visasi na mafundo ya moyoni hata katika vitu vidogo na
visivyo vya msingi, wanaweza kuzira kirahisi tena kwa muda mrefu bila
hata sababu ya msingi
4.
Wanaumizwa sana pale mwingine anapopewa pongezi au kusifiwa au kupewa
ushindi, kiu yao ni kwamba pongezi zote na sifa zote na ushindi wote uwe
wakwao. Mara mwingine anapoonekana kushinda basi wao hujifanya ndio
waliokuwa chachu au wasababishaji wa ushindi huo na kwahivyo wanataka
wapongezwe wao au mchango wao kukubalika mbele za watu


0 comments :
Post a Comment