Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini DCP Mohamed Mpinga
amesitisha utendaji wa chama cha Kutetea Abiria Taifa (CHAKUA) kuendelea
na shuguli zake katika mikoa yote nchini isipokuwa kwa mkoa wa Dar es
Salaam pekee
Akitaja sababu za kusitisha utendaji wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa ripoti ya namna walivyojipanga kuzuia ajali za Barabarani DCP Mpinga alisema,
utendaji mbaya na kukiuka maadili na kujikita katika usimamizi wa
sheria badala ya kutoa elimu unaofanywa na chama hicho ndiyo sababu ya
kusitishwa kwa utendaji wao na kwamba kuanzia sasa shughuli zao
zitafanywa na Mabalozi wa Usalama Barabarani.
Muda mfupi baada ya kutolewa kwa tamko hilo, Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Kutetea Abiria Taifa, Bwana Hassan Mchanjama
alikanusha tuhuma hizo huku akisema kuwa, kuzuia utendaji wa chama cha
abiria kwa kile alichokiita ni maslahi binafsi ni kuwanyima wananchi
mahala pa kuwasilisha kero zao ambapo amebainisha kuwa chama hicho
hakijawahi kukiuka taratibu zake za utendaji kama ilivyoelezwa.
Mbali
na suala hilo DCP Mohamed Mpinga amewataka wamiliki wa magari kote
nchini kuondoa na kuacha mara moja kutumia taa zenye mwanga mkali
maarufu kwa jina la 'Sportlights' katika vyombo vyao vya moto kwani taa
hizo ziimekuwa kero kwa madereva wengine na kuchangia ajali za
barabarani nchini.
0 comments :
Post a Comment