JESHI
la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini limesema litachukua
hatua kali kwa kuweka mahabusu madereva watakaokiuka sheria za usalama
barabarani katika kipindi hiki cha sikukuu badala ya kulipa faini kama
ilivyozoeleka.
Kauli
hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Kikosi hicho,
Mohammed Mpinga, alipozungumza na vyombo vya habari akisema kutoza
faini kumekuwa hakuwafanyi madereva kuacha kuvunja sheria.
“Kitendo
cha kutoza faini, kimekuwa kikiwafanya madereva kuvunja sheria kwa
makusudi, wakijua wakikamatwa watalipa faini na kuachwa,” alisema
Mpinga.
Mpinga
alisema katika kipindi hiki, watu wengi hupenda kusafiri kwenda maeneo
mbalimbali na hivyo kuongeza matumizi ya vyombo vya moto barabarani
ambapo pia huambatana na starehe nyingi ikiwa ni pamoja na ulevi kwa
madereva.
Alieleza
kutokana na hali hiyo ya starehe na ulevi, madereva wengi hupoteza
umakini na kushindwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hatimaye
kusababisha ajali ambazo hugharimu maisha ya watu wengi.
Alifafanua,
kwamba kipindi hiki madereva huwa na haraka na huendesha kwa mwendo
kasi, hunywa pombe, hupenda kupita magari ambayo ya mbele yao bila
hadhari na hufanya makosa ya kizembe yanayohatarisha maisha.
Kamanda
Mpinga alisema kwa kutambua hilo, wamejipanga ili kuwatia mbaroni
madereva hao na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Aidha,
alisema katika kipindi cha kuelekea mwishoni na mwanzoni mwa mwaka
mpya, wamekuwa wakifanya operesheni katika barabara zote, stendi za
mabasi ili kukagua ubora wa mabasi, mikanda, kupima ulevi madereva,
uzidishaji abiria na nauli.
Alisema
katika operesheni hii inayoendelea mikoani kwa kipindi kifupi madereva
wa mabasi ya abiria wamekamatwa kwa mwendo kasi wa zaidi ya kilometa 90
kwa saa, ambapo katika mikoa tofauti jumla ya madereva 277 walifikishwa
mahakamani wakitokea mahabusu na kulipa faini ya kati ya Sh. 300,000 na
Sh 600,000
0 comments :
Post a Comment