Kutokana na mahitaji ya usafiri katika kipindi kuelekea mwisho wa mwaka 2016 pamoja na msimu wa sikukuu, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani na pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini, SUMATRA limetangaza kutoa vibali kwa mabasi aina ya Eicher na Coaster ili kufanya safari za mikoani.
Aidha
kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama
barabarani Mohammed Mpinga pia amesema kuwa jeshi hilo limesitisha
utendaji wa chama cha kutetea abiria ‘CHAKUA’ mikoani kutokana na kukiuka maadili na kuanzia sasa watabaki na watendaji wa kituo cha mabasi Ubungo pekee.
“Tumeamua
kutoa vibali kwenye mabasi mengine ili kurahisisha usafiri kutokana na
kuanza kuongezeka kwa abiria, mfano juzi kwenye kituo cha Ubungo
yalitoka mabasi 421, jana yametoka mabasi 470 sasa tumeamua kuongeza na
Coaster na tumeshafanya ukaguzi mabasi yote yako salama” – Kamanda Mpinga


0 comments :
Post a Comment