SOURCE BBC
Adama Barrow, mtu aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Gambia ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo.
Alikula kiapo hicho katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal huku akiwaagiza wanajeshi wa Gambia kusalia katika kambi zao.
Ametambuliwa kimataifa.
Lakini aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh amekataa kujizulu na muda wake wa kuhudumu umeongezwa na bunge.
Viongozi wa Afrika Magharibi wameshindwa kumsihi bw Jammeh kuondoka mamlakani.
Wametishia kumuondoa kwa nguvu.
Bw Jammeh alishindwa katika uchaguzi huo wa Disemba mosi ,kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Lakini anataka matokeo ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali akidai makosa mengi katika uchaguzi huo.
”Mimi Adama Barrow ,naapa kwamba
nitatekeleza wajibu wangu katika afisi ya urais wa taifa la Gambia
kwamba nitahifadhi na kutetea katiba” .
Na katika hotuba yake ya
kuapishwa ,aliwaagiza wanachama wote wa jeshi la gambia kusalia katika
kambi zao. ”Wale watakaopatikana wakibeba silaha watachukuliwa kuwa
waasi”, alionya.
0 comments :
Post a Comment