
Jammeh ameondoka kwa Ndege kwenye taifa hilo na hii picha hapa chini inamuonyesha akiwa anaingia kwenye Ndege na akipungiwa mikono ya byebye na baadhi ya Wafuasi wake ikiwa ni muda mfupi baada ya Bendi ya Jeshi kutumbuiza.
Wakati wote huo Jammeh alionekana akiwa na kitabu kitakatifu cha Koran na alitumia mkono huohuo ulichokibeba kuwapungia waliojitokeza uwanja wa ndege kumuaga huku ikiaminika anakwenda Guinea kwa sasa wakati akisubiri kuhamia moja kwa moja kwenda kuishi kwenye taifa jingine.
BBC wameripoti kwamba wakati anaondoka uwanja wa ndege Wafuasi wake na baadhi ya Wanajeshi walionekana kuhuzunika na hata wengine kutokwa machozi lakini mitaani wengi wamefurahia kuondoka kwake akiwa ni Rais wa kwanza wa Gambia kuachia madaraka kwa amani toka ilipopata Uhuru mwaka 1965.

Yahya ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 22, saa chache baada ya matokeo kutangazwa alikubali kushindwa lakini baadae akabadili mawazo na kusema amehujumiwa na kwamba yeye ndio mshindi hivyo akaendelea kung’ang’ania madaraka.

Jammeh akiwa kwenye Ndege akiondoka Gambia
Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ulimuamuru Jammeh kuachia madaraka kabla ya saa sita mchana lakini mwenyewe akaomba aachie madaraka ifikapo saa kumi jioni na kweli ametekeleza.

Picha nyingine ikimuonyesha akiwa ndani ya Ndege tayari kwa kuondoka

Kwenye mji mkuu baadhi ya Raia wa Gambia wameanza kusherehekea kuondoka kwa Jammeh.

0 comments :
Post a Comment