CHADEMA kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mbunge wake kwenda jela miezi sita


Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema kuwa chama hicho kitakata rufaa dhidi ya hukumu ya kwenda jela miezi sita ya Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mheshimiwa Peter Lijualikali wa CHADEMA, iliyotolewa leo na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero,mkoani Morogoro. Tundu Lissu amekiambia kituo cha Radio cha EFM 93.7DSM kwamba, hukumu hiyo ni mwendelezo wa dhuluma dhidi ya wapinzani nchini. Amesema CHADEMA, pia watamwekea dhamana mbunge huyo ya kuwa nje wakati rufaa ikishughulikiwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment