Na.Alex Mathias
Licha ya kufungwa kwa penati na
Ghana timu ya Uganda imeonesha kiwango cha hali ya juu na kuweza
kuwafunika wachezaji wa Black Stars wanaocheza Ligi za Ulaya mchezo wa
Kundi D wa Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ uliomalizika
katika uwanja wa Stade De Port-Gentil uliopo Mji wa Port-Gentil nchini Gabon.
Beki Asaac Isinde dakika ya 30 ndiye aliyeigharimu Uganda baada ya kumchezea rafu mbaya mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan ndani ya box na mwamuzi kuamuru ipigwe penati na mshambulizi wa West Ham inayoshiriki ligi ya Uingereza Andrew Ayew alipingilia msumari huo.
Baada ya kufungwa goli hilo The Cranes walianza kucheza mchezo wa kufunguka na kuona hata hivyo Uimara wa Mlinda mlango Denis Onyango uliwanyima magoli mengi Ghana na mpaka mapumziko Blacks Stars walienda kifua mbele.
Kipindi cha pili timu zote
zilifanya mabadiliko hata hivyo Uganda waliweza kuwakamata Ghana kipindi
cha pili na kuweza kuwapa nafasi nyingi za wazi na kama Nahodha Simon Massa basi matokeo yangekuwa tofauti.
Baada ya kuona kuwa wanashambuliwa kocha wa Ghana Avram Grant
alianza kucheza mchezo wa kujilinda na kushambulia hata hivyo vijana wa
kocha wa zamani wa mabingwa watetezi wa Vodacom Tanzania Yanga,Milutin SREDOJEVIC waliweza kuutawala mchezo.
Washambuliaji wawili wa Uganda
Simon Massa na Farouk Miya ndo wameiangusha safu ya ushambuliaji wa The
Cranes hivyo mechi inayokuja kocha anatakiwa kuisuka upya zaidi ili
waweze kushinda
Mpaka dakika 90 zinamaliza Ghana
wameibuka na ushindi wa goli 1-0 na kuwafanya waongeza kundi hilo huku
Mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 4:00 kwa saa za Afrika
Mashariki ambapo mabingwa wa kihistoria wa Michuano hiyo timu ya Misri
itacheza na Mali.


0 comments :
Post a Comment