Kahama: Mkuu Wa Wilaya Awapiga Marufuku Walimu Kuzuia kuandikisha Wanafunzi Kisa Vyeti vya Kuzaliwa

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu amewapiga marufuku walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari kuzuia kuandikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza hadi wawe na vyeti vya kuzaliwa. 

Nkurlu alitoa agizo hilo baada ya baadhi ya wazazi na wanafunzi kufika ofisini kwake kusaka vyeti na wengine kulalamika kitendo cha walimu kuwazuia kuanza kidato cha kwanza.

“Ni marufuku kwa mwalimu yeyote au kiongozi kuzuia wanafunzi kuandikisha kwa madai ya cheti cha kuzaliwa kama wanataka kujiridhisha wapate barua kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji au watendaji wa kijiji na siyo cheti hicho,” alisema Nkurlu.

Mmoja wa maofisa elimu kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama, Aruko Lukolela alisema agizo la mkuu wa wilaya litatekelezwa mara moja. 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment