Msimuliaji : Dokta. mungu wa kabili …….0744 000 473
Asalaam Aleykum Ndugu zanguni. Habari za mwaka mpya wa 2017.
Ni matumaini yangu kuwa Mwenyezi Mungu amewavusha salama.
Niende
kwenye mada ya leo, Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipata kesi za
watu ambao nikiwatazama katika jicho la rohoni, nagundua ya kwamba,
matatizo yao yanahusiana moja kwa moja na kutofuata ama kutozingatia
miiko ya jinsi ya kushughulika na habari za wafu.
Ninapo
zungumzia habari za wafu, namaanisha masuala yoote yanayo husiana
na wafu, kuanzia makaburi, maiti, vyumba vya kuhifadhia maiti, taratibu
za kumuandaa na kumuosha marehemu, taratibu za maziko na mazishi,
taratibu za matanga & maombolezo, nguo za marehemu, masuala ya
mirathi ya marehemu, jinsi ya kuishi na yatima walio achwa na marehemu,
mke au wake za marehemu , mali za marehemu nakadhalika.
Watu
wengi wana pata nuksi, mikosi au hata vifo visivyo vyao, kwa sababu ya
kutozingatia taratibu za namna ya kushughulika na wafu.
Somo
hili lina muhusu kila mmoja wetu, kwa sababu kila mtu anaweza
kupata msiba wa ndugu, jamaa au rafiki wakati wowote ule.
Pamoja
na kwamba, hakunaga mtu mwenye uzoefu wa kufiwa. ( Yaani
kuzoefu uchungu wa kufiwa kwa sababu umeshapata misiba mizito
mingi ), lakini linapokuja suala la kufahamu kuhusu miiko na
taratibu za namna ya kushughulika na habari za wafu, kila mtu
anapaswa kuwa na uzoefu wa kutosha, kwa sababu msiba unaweza
kuja wakati wowote.
Ni
muhimu sana kujua taratibu na miiko ya namna ya kushughulika na habari
za wafu ili usije kupata madhara yasiyo ya lazima, kwa sababu ya
kutokujua nini cha kufanya pale unapokuwa una shughulika na habari za
wafu.
Kwa
bahati mbaya sana, nyakati za siku hizi hata watu wazima nao hawajui
namna ya kushughulika na habari za wafu. Kupitia mfululizo wa makala
haya, nitakuwa nikielezea kuhusu miiko mbalimbali ya namna ya
kushughulika na habari za wafu.
Fuatilia
makala haya mwanzo hadi mwisho, ili upate kuzijua taratibu hizo na
hivyo kujiepusha na madhara mbalimbali yanayo weza kukupata kutokana na
kutokujua kwako.
1. KAMA UMEJIFUNGUA MTOTO AMBAE AMEZALIWA AKIWA AMESHA KUFA TAYARI
Moja
kati ya mambo ambayo unapaswa kuwa nayo makini sana, ni pale unapokuwa
una shughulika na mazishi ya kichanga, hususani kile kilicho zaliwa
kikiwa kimekufa tayari.
Hii
ni kwa sababu, maiti ya vichanga, pamoja na eneo vinapozikwa vitoto
vichanga ni hazina kubwa sana katika ulimwengu wa wachawi na walozi.
Katika
ulimwengu wa wachawi na walozi, watoto wachanga walio zaliwa wakiwa
wamekufa tayari, hujulikana kama “ WATU WALIO PITA DUNIANI BILA
KUONEKANA” .
Wachawi
wanapo sikia mwanamke amejifungua kitoto kichanga kikiwa kimefariki
dunia, hukusanyika na kufanya karamu kubwa ya kichawi, kwa sababu ,
maiti ya kitoto kichanga kilicho zaliwa kikiwa kimefariki dunia, ina
maana kubwa sana katika shughuli zao.
Wachawi
hutumia vitovu vya watoto wachanga walio zaliwa wakiwa wamekufa, kama
malighafi ya kutengeneza aina mbalimbali za ndumba za kichawi, mfano;
kutengeneza ndumba ya kuwafanya wasionekane na maadui zao, kutengeneza
uchawi wa kuiba na kufunika nyota ya mtu au biashara ya mtu na kumfanya
mtu huyo pamoja na biashara yake visonekane hadi anaingia kaburini,
kutengeneza mafuta yajulikanayo kama mafuta ya usiku, ambayo hutumiwa na
wafanyabiashara hasa wafanya biashara ndogo ndogo katika kuvuta wateja
kwenye biashara, kutengeneza filimbi ya kichawi ambayo hutumika kuwaita
wachawi kwenye mikutano yao ya kichawi.
Wachawi
hutumia kufanya matambiko mazito kwenye makaburi yaliyo tumika kuzika
vitoto vichanga ambayo mara nyingi huwa yanakuwa majumbani.
Matambiko
hayo ya kichawi, huwa na madhara makubwa sana kwa watu wanaoishi katika
nyumba hiyo, hususani wazazi pamoja na ndugu wa hicho kichanga.
Endapo
wachawi watafanikiwa kutumia katika shughuli zao za kichawi, maiti ya
kichanga kilicho zaliwa kikiwa kimekufa, mabalaa, nuksi na mikosi
mbalimbali itaiandama familia ya kichanga hicho, kwa sababu moja kati ya
maunizi yanayo fanywa na wachawi, huwa ni pamoja na kuwatupia mikosi
wazazi wa kichanga hicho, hususani mama wa kichanga hicho.
Wachawi
watatumia tambiko la kitoto hicho kichanga kama lango la kichawi la
kuingia katika familia ya wazazi wa kitoto hicho na kuifanya kama
watakavyo.
Moja
kati ya dalili kwamba, wachawi wametumia katika shughuli zao za
kichawi, kitoto chako kilicho zaliwa kikiwa kimekufa, ni pamoja na
kutopata ujauzito , kubeba mimba zinazochoropoka, au kuendelea kuzaa
vitoto vilivyo kufa, katika kila ujauzito unao upata.
NINI
CHA KUFANYA : 1. Kwanza unapokuwa mjamzito unatakiwa kuchukua tahadhari
ya hali ya juu sana ili kuepuka kuzaa kitoto ambacho kimekufa, kwa
sababu wachawi huwa wanawafunga wanawake wajawazito wajifungue vitoto
vilivyo kufa ili waweze kuvitumia katika mambo yao ya kichawi.
Hivyo
unapokuwa na mke mjamzito, hakikisha unampa kinga madhubuti ambayo
itawazuia wachawi kumfunga na kusababisha kichanga hicho kisicho na
hatia, kuzaliwa kikiwa kimepoteza maisha. 2. Kama tayari umejifungua
kitoto ambacho kimezaliwa kikiwa kimeshakufa, unatakiwa ufuate taratibu
maalumu za kukifanyia maziko maalumu, pamoja na wewe mwenyewe kufanyiwa
tambiko maalumu la kukusafisha na kukukinga dhidi ya jambo kama hilo,
katika siku zako zijazo.
Taratibu
za maziko ya vitoto vichanga vilivyo zaliwa vikiwa vimekufa,
zinategemea na mambo makuu yafuatayo : jinsia ya mtoto, siku aliyo
zaliwa mtoto, mtoto amezaliwa peke ake au wamezaliwa mapacha, kama ni
mapacha wamekufa wote au mmoja amepona, na kama mmoja amepona, zipo pia
taratibu za namna ya kumfanyia tambiko na ibada maalumu ili kumuepusha
na jicho la maadui wa kichawi.
Kitu
kingine, inategemea na mtoto aliyezaliwa ni NZAO ama UZAO wa ngapi wa
mwanamke aliye jifungua. Kama ni uzao wa kwanza, kuna taratibu zake, na
kama ni uzao wa mwisho kuna taratibu zake pia.
Taratibu hizi zisipo fuatwa, basi madhara makubwa sana yatatokea kwa familia husika.
2. KAMA MAMA AMEFARIKI NA MTOTO AMEBAKI HAI
Kama utapatwa na mtihani huu, unapaswa kuwa makini sana na kuzingatia taratibu na kanuni za kufuata.
Ninaposema
kuwa makini namaanisha uwe makini kwelikweli, kwa sababu wachawi wana
siri kubwa sana na mwanamke aliye jifungua na kufariki dunia.
Kuwa
makini sana na watu watakao enda kuuosha mwili wa mke wako ,au dada
yako n.k ambae amefariki wakati anajifungua, kwani baadhi yao watakuwemo
wachawi ama mawakala wa wachawi ambao watachukua baadhi ya vitu vya mke
wako na kwenda kuviuza kwa wachawi.
Vitu hivyo ni pamoja na nywele, nywele za sehemu za siri, kucha, na maji yaliyo tumika kumuoshea.
Vitu
hivyo hutumiwa na wachawi kutengeneza ndumba za aina mbalimbali, kama
vile kuwafunga wanafunzi wanao soma, wafanyakazi, wafanya biashara
nakadhalika.
3. KAMA MAMA NA MTOTO WOTE WAMEFARIKI:
Kama
kwa bakti mbaya umepatwa na mtihani mzito kama huu, unapaswa kuwa
makini na kuchukua tahadhari kama ilivyo elezwa hapo juu.
4. KAMA NDUGU YAKO ALIYE FARIKI ALIKUWA KICHAA AU MWENDAWAZIMU
Kama
ndugu yako aliyefariki alikuwa kichaa au mwendawazimu wakati wa uhai
wake na alifariki dunia akiwa katika hali hiyo unapaswa kuzingatia
yafatayo :
Kwanza
maiti yake isilale ndani. Itoke moja kwa moja mochwari hadi makaburini.
Nguo zake zote zichomwe moto siku ya saba baada ya maziko.
Kuweni makini sana na watu watakao enda kuosha mwili wake.
Ikiwezekana
awepo mwanafamilia anae aminika, wakati wa zoezi la kuuosha mwili wa
ndugu yenu, kwa sababu watu walio kufa wakiwa wendawazimu ni hazina
kubwa sana kwa wachawi, kuanzia sehemu za miili yao, hususani nywele na
kucha, nywele za siri , sanda iliyo tumika kuwavisha, nguo walizokuwa
wamevaa wakati wa kupatwa na umauti pamoja na kaburi lililo tumika
kuwazika.
Wachawi hutumia vitu hivyo katika kutengeneza uchawi na ulozi wa aina mbalimbali.
Kwa
mfano, nywele za marehemu ambae alikuwa mwendawazimu wa jinsia ya
kiume, hutumika kutengeneza ndumba ya kichawi ya kumtuliza kimapenzi
mwanaume na kumfanya awe kama mwendawazimu kwa mwanamke aliye mfanyia
uchawi huo.
Vivyo
hivyo, nywele za mwanamke aliyefariki akiwa mwendawazimu hutumika
kutengeneza uchawi wa kuwapumbaza wanawake kimapenzi na kuwafanya kuwa
kama wendawazimu kwa waume zao.
Kama
hiyo haitoshi, wachawi huchukua nywele za marehemu mwendawazimu wa
kiume, huchanganya na nywele za mwendawazimu mwanamke, nywele za mtu
aliyekufa akiwa msukule, mafuta ya msukule pamoja na ndumba nzingine,
ili kutengeneza uchawi wa kuwapumbaza na kuwafunga wafanyakazi hususani
wale wanao fanya kazi kwenye kampuni za watu binafsi.
Uchawi huu hutumiwa sana na matajiri wanao miliki maduka, hoteli, migahawa au kampuni zao binafsi.
Mtu
aliye fanyiwa uchawi huu mara nyingi huwa na uwezo mkubwa na wa kipekee
katika kazi yake, na bosi wake anakuwa hayupo tayari kupoteza huduma
yake, basi anacho kifanya ni kumlisha uchawi huu na kumpumbaza katika
maisha yake yote.
Vilevile, wachawi hutumia vitu vya mwendawazimu kutengeneza uchawi wa biashara hususani biashara ya chakula .
Mtu
ukishakula tu chakula kilicho wekwa uchawi huu basi utakuwa kama
mwendawazimu kwenye chakula cha kwenye mgahawa au hoteli hiyo.
Huwezi kula chakula sehemu nyingine yoyote ile isipokuwa kwenye mgahawa huo tu, hata yatokee mabadiliko gani.
Uchawi
huu pia hutumiwa na wafanyabishara wa biashara nyinginezo kama vile
nguo nakadhalika. Kumpumbaza mteja. Mteja huweza kununua nguo ambayo
thamani yake ni sh elfu kumi, kwa shilingi laki moja.
Uchawi
huo ndio unao tumiwa sana na akina dada katika kuwapumbaza wanaume na
kuwafanya wawape kila kitu wanacho kitaka. Endapo utaruhusu wachawi
watumie vitu vya marehemu ndugu yenu ambae amefariki akiwa mwendawazimu,
basi mikosi na mabalaa makubwa yataiandama familia yenu.
5. KAMA NDUGU YAKO ALIYE FARIKI ALIKUWA KIPOFU !
Unapaswa kuwa makini sana, pale unapopatwa na msiba wa ndugu yako wa damu ambae alikuwa na ulemavu wa kutokuona yaani kipofu.
Hii
ni kwa sababu wachawi wanaweza kutumia katika shughuli zao za kichawi
baadhi ya vitu vya ndugu yenu na matokeo yake kuiacha familia yenu ikiwa
kwenye mabalaa na mikosi isiyo elezeka.
Kuweni makini sana na aina ya watu watakao pewa jukumu la kuosha mwili wa ndugu yenu.
Nawashauri
badala ya kuwapa kazi hiyo watu wa mochwari, ifanye ninyi wenyewe ili
kuhakikisha kuwa hakuna ufisadi wowote unao fanyika hapo.
Kwani
endapo hamtafanya hivyo, basi mtatoa nafasi kwa wachawi pamoja na
wakala wao kuchukua baadhi ya vitu vya ndugu yenu huyo kwa ajili ya
kufanya shughuli zao za kichawi.
Vitu
hivyo ni pamoja na nywele, nyusi,nywele za siri,kucha, nguo alizokuwa
amezivaa marehemu wakati anaaga dunia, kama alikuwa anatumia gongo la
mti, nalo ni dili kubwa sana kwa wachawi, maji yaliyo tumika kumuosha
nakadhalika.
Pamoja
na mambo mengine, vitu vya marehemu ambae wakati wa uhai wake alikuwa
na ulemavu wa kuona yaani upofu ( Hasa Yule aliye zaliwa na upofu ),
hutumiwa na wachawi kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile
uchawi wa kuwafunga maadui zako wasi kuone, uchawi wa mapenzi kumfanya
mpenzi wako asimuone mtu mwingine yoyote Yule isipokuwa wewe tu, kufunga
nyota ya mtu isionekane na yoyote Yule. Kwenye kaburi la marehemu
aliyekuwa na ulemavu wa kuona, hufanyika tambiko la kuzika na kufunga
kesi, kuifanya isionekane.
Pia vitu hivyo hutumika kuwaloga wanawake wajawazito kuzaa watoto wenye ulemavu wa macho
6. KAMA NDUGU ALIYE KUFA ALIKUWA NA ULEMAVU WA KUTOSIKIA :
Wachawi
hutumia vitu vya mtu aliye fariki ambae wakati wa uhai wake alikuwa na
ulemavu wa kusikia, kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile;
Mapenzi; kumfanya mpenzi asisikie jambo la mtu yoyote Yule, isipokuwa
wewe tu, kumroga mtoto wa mtu kumfanya asiwasikie wazazi wake, kumroga
mke au mume wa mtu kufanya asiwe na masikizano na mwenzi wake
nakadhalika.
Vitu
vinavyo tumika hapo ni pamoja na nywele, nyusi, kucha, nywele za siri,
nguo zake, maji yalotumika kumwosha pamoja na kaburi lake.
Unapopatwa na msiba wa ndugu ambae wakati wa uhai wake alikuwa na tatizo la ulemavu wa kusikia, basi unapaswa kuwa makini sana.
7.
KAMA NDUGU YENU AMEKUFA MAJI : Kama mmepata taarifa kuhusu msiba wa
ndugu yenu ambae amekufa maji, eidha alikuwa anaogelea, au amepata ajali
kwenye mashua au jahazi au meli, zipo taratibu na miiko ya kufuata
wakati wa maziko yake.
Moja ya miiko hiyo ni pamoja na “ msichimbe kaburi kabla hamjaupata mwili wa marehemu”.
Hakikisheni
kwanza mmeupata mwili wake ndio mchimbe kaburi na kumzika kwa kufuata
taratibu zote za kumzika mtu aliye fariki kwenye ajali ya maji.
Msichimbe
kaburi kabla hamjauona mwili wa marehemu. Endapo mtachimba kaburi kabla
ya kuuona mwili wa marehemu halafu ikatokea bahati mbaya msiupate mwili
wa marehemu, basi kwanza, mmoja kati ya ndugu wa karibu katika
familia ya marehemu, atafariki dunia ndani ya mwaka huo huo.
Idadi ya ndugu watakao fariki ndani ya mwaka mmoja,
itategemeana na idadi ya siku ambazo hilo kaburi limekaa wazi.
Kama hiyo haitoshi, pili , mtakuwa mmewapa faida kubwa sana wachawi.
Wachawi wataenda kulitumia kaburi hilo kutengeneza uchawi mkubwa na wenye nguvu sana.
Makaburi
ya namna hiyo hapa Afrika mashariki yapo machache sana, na yanapatikana
zaidi nchini Congo DRC na Tanzania hususani kanda ya ziwa na kanda ya
kusini katika mkoa wa Lindi.
Kanda
ya ziwa makaburi hayo yapo katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu,
na mengi kati yao ni yale ya wahanga wa ajali ya meli ya MV Bukoba ya
mwaka 1996, ambapo mamia ya miili ya abiria waliokuwa kwenye meli hiyo
haikuweza kupatikana, ilihali ndugu, jamaa na marafiki walisha chimba
makaburi.
Huko
nchini Kongo, idadi kubwa ya makaburi hayo ni yale ya wale mabinti
bikira, walio kufa kwenye ajali ya meli iliyotokea mto Kongo miaka ya
70.
Katika
ajali hiyo hakuna, mwili uliopatikana hata mmoja na idadi kubwa ya
ndugu, jamaa na marafiki wa mabinti hao ilikuwa tayari imeshachimba
makaburi kwa ajili ya kuwahifadhi wapendwa wao hao. LAWAMA NYINGI KUHUSU
AJALI HIYO ZILIELEKEZWA KWA ALIYE KUWA RAIS WA KONGO KIPINDI HICHO,
MOBUTU SSESESEKO AKIDAIWA KUWATOA KAFARA MABINTI HAO KWA MAELEKEZO YA
KAMATI YAKE YA UFUNDI ( Miiko yangu ya kazi, hainiruhusu kutoa maoni
yangu kuhusu jambo hili )
8.
MSICHIMBE KABURI HALAFU LIKALALA BILA KUZIKWA : Kaburi huwa halilali
njaa, hakikisheni siku mtakayo chimba kaburi hilo, iwe ndio siku
mtakayo mzika marehemu wenu.
Kamwe msichimbe kaburi kabla mwili haujafika nyumbani.
Endapo mtakiuka jambo hilo, basi misiba itaiandama familia yenu kwa mwaka mzima.
Mtakuwa
mmeiunganisha familia yenu na kaburi lililo lala wazi kwa
hiyo siku moja. Tumbo la kaburi hilo litadai malipo yake ya kulala
bila chakula chake kwa siku nzima.
9. MSIACHE KABURI WAZI WAKATI MNAENDA KUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU
Mkishamaliza
kuchimba kaburi, msilitelekeze peke yake. Wekeni watu kadhaa wa kulinda
kaburi ambao watakaa huko kaburini hadi pale mwili wa marehemu utakapo
letwa kuzikwa.
10. MWANAMKE MJAMZITO ASIHUDHURIE MAZISHI Mwanamke mjamzito hatakiwi kuhudhuria kwenye maziko ( makaburini ).
Endapo
atafanya hivyo basi, roho ya marehemu itamuingia mtoto aliyeko tumboni,
na hivyo kusababisha bahati mbaya na mikosi kwa mwanamke huyo wakati wa
kujifungua na endapo atajifungua salama, basi mtoto atakae zaliwa
anaweza kupoteza uhai, au endapo ataishi basi, mama huyo atafariki
na kumuacha motto na motto atakuwa kwa taabu sana na ataandamwa na
mikosi.
Kama
itatokea mwanamke huyo akalazimika kuhudhuria kwenye mazishi ( Mfano
labda aliyefariki ni mtu wake wa karibu sana kama vile mama yake,baba
yake, mume wake, kaka yake, dada yake au mtoto wake ), basi anatakiwa
ASITAZAME MWILI WA MAREHEMU wakati wa kuaga.
Endapo
atafanya hivyo, basi ile roho ya marehemu itaishaishawishi roho ya
mtoto aliyepo tumboni, kwenda kwenye nchi ya wafu, jambo ambalo
litasababisha matatizo makubwa sana kwa mama wa mtoto wakati wa
kujifungua.
Uwezekano wa kujifungua mtoto aliyefariki, utakuwa kwa asilimia mia.
11.
Unapopita kwenye eneo la makaburi mida ya saa saba mchana au saa moja
usiku, usiache mdomo wako wazi wala kupiga miayo. Endapo utafanya hivyo,
roho za wafu zitakuingia na kusababishia matatizo makubwa.
12. Mnapomzika marehemu, kichwa kiangalie upande wa magharibi na miguu iwe upande wa mashariki.
14.
Mara tu kifo kinapotokea, kitu cha kwanza, unacho takiwa ni kuondoa ama
kufunika picha na vioo vyote vilivyomo kwenye chumba alichopo marehemu.
Ni nuksi kubwa sana kuacha taswira ya mwili wa marehemu ionekane kwenye
kioo. Kama hiyo haitoshi, ni nuksi kubwa sana kutazama taswira yako
kwenye kioo hicho, mpaka mwili wa marehemu uatakapo kuwa umeondolewa.
Ukitaka kuamini ninacho kisema, jaribu kuingia na kioo kwenye chumba
alimo lala marehemu halafu jitazame kwenye hicho kioo. Utakacho kiona,
uje ukisimulie hapa.
15. Naweni mikono kwa dawa maalumu baada ya kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu.
16. Oga dawa mara baada ya kutoka kaburini.
17.
Kama marehemu amefariki akiwa nyumbani, mnapoenda kuutoa mwili wake,
miguu itangulie kutoka, kamwe msifanye kosa mkatanguliza kichwa.
18.
Kama watu wawili katika nyumba moja, wanaumwa sana, halafu ikatokea
mmoja wao akafariki dunia, basi hiyo ni ishara kwamba huyo mwingine
atapata nafuu kubwa.
19.
Kuna ndege mmoja anapatikana porini ( SIMTAJI KWA SABABU ZA KIMIIKO),
ukichukua nyoya la huyo ndege halafu ukaliweka kwenye mto wa kitanda
anacho lalia mgonjwa, basi mgonjwa huyo atakufa wala hatopona. Nyoya
hilo hilo likiwekwa kwenye kitanda anacholalia mtoto mdogo, litamzuia
mtoto huyo kukua.
20.
Kitanda anacho lalia mgonjwa mahututi, kitazame mashariki na magharibi,
na kamwe sio kaskazini na kusini. Kichwa kiangalie magharibi na miguu
itazame mashariki.
21. Jina la mwisho kutajwa na marehemu wakati anakaribia kukata roho, litakuwa jina la mtu atakae fuatia kufa baada ya marehemu.
22.
Endapo mtu anae karibia kukata roho, atakun’gata, basi na wewe
utamfuata baada ya muda mfupi. Ili kujiepusha na kifo cha namna hiyo,
basi unatakiwa na wewe umng’ate katika sehemu ile ile aliyo kun’gata.
23.
Kama kiongozi wa familia atafariki dunia, basi mnatakiwa kusimamisha
saa kubwa ya ukutani inayo kaa sebuleni, vinginevyo wanafamilia walio
baki nao watamfuata ndani ya kipindi kichache, vitatokea vifo mfululizo
vya wanafamilia.
24.
Baada ya kuuosha mwili wa marehemu, na kuuvisha nguo zake, unatakiwa
kuweka punje moja ya chumvi kwenye kifua cha marehemu ili kuwafukuza
roho na majini wabaya.
25.
Kama marehemu atakuwa akiwa ameacha macho wazi , hiyo ni ishara mbaya
sana. Maana yake ni kwamba,anatafuta watu ( ndugu zake ) wa kwenda nae
kaburini. Kujiepusha na hilo, funikeni macho yake kwa kutumia sarafu .
26.
Usifagie chumba cha marehemu kabla marehemu hajatolewa. Endapo utafanya
hivyo, basi amini nakwambia wewe ndie utakae mfuata marehemu.
27.
Msitoe shuka wala nguo yoyote iliyopo kwenye kitanda alicho kilalia
marehemu, na ambacho umauti ulimkuta. Endapo mtakiuka hilo, basi
mwanafamilia mwingine atafariki ndani ya mwaka huo huo.
28.
Endapo Kundi la wanandugu, jamaa na marafiki, mtaenda kuuchukua mwili
wa marehemu halafu ghafla mkaona anatoa damu kwenye tundu za pua, basi
mjue kuwa marehemu amekufa kwa mkono wa mtu, na aliye husika na kumuua,
yu miongoni mwenu,ndani ya chumba hicho hicho.
29.
Kwa mara nyingine tena narudia, mwili wa marehemu unapotolewa kwenye
jengo lolote lile, iwe nyumbani, kanisani, au msikitini ni lazima miguu
ndio itangulie kutoka na sio kichwa, vinginevyo roho au mzimu wa
marehemu huyo, utatazama katika jengo hilo na kumuita mtu mwingine wa
kufuatana nae.
30.
Marehemu azikwe mahali alipo pachagua wakati wa uhai wake, au la sivyo
endapo mtaenda kinyume chake, vifo vitatokea katika familia hiyo. Na
kama mtalazimisha kusafirisha mwili wa marehemu, basi msafara huo lazima
utapata ajali njiani, na mtu mmoja lazima atakufa.
31.
Ukiugusa mwili wa marehemu, utakuwa na uhakika kwamba, roho ya marehemu
haitakusumbua. Na endapo utaugusa mwili wa marehemu usoni, hutoota
ndoto mbaya kuhusu marehemu huyo.
32.
Usipeleke mwili malaloni kwa kutumia gari lako binafsi. Ni nuksi kubwa
sana kufanya hivyo. Mwili wa marehemu unapelekwa malaloni kwa kutumia
gari maalumu.
33. Endapo mtasafirisha mwili wa marehemu kwa basi, kichwa kitazame anapotoka na miguu itazame anapoelekea.
34. Usi hesabu magari kwenye maziko (makaburini), ukifanya hivyo unakuwa unahesabu siku zako mwenyewe za kuishi.
35.
Kuwa muangalifu usione taswira yako kwenye gari lililo beba mwili wa
marehemu, vinginevyo wewe ndio utakae fuatia kubebwa kwenye gari hilo.
36. Usiende na mtoto mchanga kwenye msiba, vinginevyo atakufa kabla hajatimiza mwaka mmoja.
37.
Ni nuksi kubwa sana kutangulia makaburini ( kwenye maziko) au kupita
bila kushiriki kwenye maziko . Kama utafanya hivyo, utakufa ndani ya
muda si mrefu.
38.
Kama paka mweusi atakatisha mbele wakati wa maziko (makaburini )
mwanafamilia mmoja katika familia ya marehemu atakufa ndani ya siku
tatu.
39.
Kama ndugu yenu amekufa, kwa kuuwawa au mna wasiwasi kwamba ndugu yenu
ameuwawa, basi mzikeni huku kichwa kikiwa kinatazama chini. Mtu aliye
muua ndugu yenu, kama atakuwa kwenye eneo la maziko, basi hatoondoka
eneo hilo hadi atakapo kamatwa. Watu wote wataondoka, lakini yeye
atabaki, hapo hapo, atakuwa kama amepagawa na kupigwa na bumbuwazi.
Kama msiporudi kutazama hapo kaburini, basi hata siku tatu mtamkuta, na
atakapo waona, basi ata tubu na mtafikisha kwenye vyombo vya dola.
Miaka
ya sabini kushuka chini, babu zetu ilikuwa kama ndugu yao amekufa kwa
kuuwawa ama kama wanahisi ndugu yao amekufa kwa kuuwawa, mfano amewekewa
sumu, amenyongwa n.k,. basi walikuwa wanafanya hivi, wanatoa ini la
marehemu, halafu wanazika ini sehemu tofauti na mwili wa marehemu, kwa
kufanya tambiko maalumu. Ndani ya siku saba, mtu aliye muua marehemu,
atapatikana katika eneo lililozikwa ini.
40.
Kaburi lilisale wazi, likilala wazi, basi mwanafamilia mwingine katika
familia ya marehemu atafariki ndani ya mwaka huo huo. Kaburi lizikwe
siku liliyo chimbwa.
41.
Kaburi likilala wazi siku ya Jumapili, basi jumapili itakayo fuata,
mwanafamilia mwingine kutoka kwenye familia ya marehemu na yeye
atamfuata marehemu.
42.
Vifaa vilivyo tumika kuchimba kaburi, vinatakiwa vibakie kaburini kwa
siku nyingine saba. Kuvipeleka nyumbani vifaa hivyo siku hiyo hiyo aun
kabla ya siku saba, ni nuksi kubwa sana.
43.
Kuondoka makaburini kabla kaburi lote halijafukiwa, kutasababisha msiba
kwenye familia yako wewe uliye ondoka kabla watu hawajamaliza kuzika.
Mvua ikinyesha kwenye kaburi ambalo bado halijafukiwa, ni ishara mbaya
sana kwa familia ya wafiwa. Ili kuepukana na nuksi hiyo, inabidi
kuwe na mtaalamu wa kuzuia mvua.
44. Ni nuksi kubwa sana kusonta kaburi
45. Ni nuksi kubwa sana kurukia kwenye kaburi
46. Ni nuksi kutembelea makaburini baada ya jua kuzama
47.
Wafiwa wasiondoke nyumbani wala kujichanganya mtaani na watu
wengine, hadi matanga yatakapo inuliwa. Kwa mfano watu wengine,
unakuta mtu amefiwa, lakini kabla hata matanga hayajainuliwa,
anakwenda bar kunywa na kurudi msibani. Hayo ni makosa makubwa
sana.
48.
Wafiwa wote wakuu, yaani ndugu wa karibu wa marehemu, wasioge
hadi baada ya siku tatu, ambayo ndio siku ya kuanua matanga,
na maji watakayo oga yawe maji ya moto.
49. Wafiwa wasishiriki ngono hadi matanga yatakapo inuliwa.
50. Waombolezaji msibani, wasiongee kwa nguvu wala kucheka kwa nguvu. Ni makosa makubwa sana kufanya hivyo.
Leo
tumekomea miiko 50. Kama kichwa cha maya kinavyo jieleza, MIIKO
ELFU MOJA NA MOJA YA WAFU. Hivyo basi, ili kufahamu kuhusu
miiko mingine iliyo baki, tembelea kila siku:
www.mungwakabili.blogspot.com
Imesimuliwa na Dokta. mungu wa kabili. Anapatikana kwa simu namba 0744 000 473
0 comments :
Post a Comment