Raundi ya tano ya mechi za kuwania
Kombe la Shirikisho la Azam 2016/17 (Azam Sports Federation Cup –
ASFC), utaanza Jumamosi Januari 21, 2017 kwa timu za Majimaji na Mighty
Elephant za Songea kucheza kwenye Uwanja Majimaji mjini Songea.
Ratiba ya ASFC inaonesha kwamba
timu za Alliance na Mbao za Mwanza zitacheza pia keshokutwa Jumamosi
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati Young Africans itacheza na Ashanti
United kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Jumapili Januari 22, mwaka huu
Ruvu Shooting itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mabatini
ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Toto Africans itacheza na Mwadui ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Simba
itakipiga na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam
kadhalika Mbeya Warriors ikicheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya.
Jumatatu Januari 23, mwaka huu
Stand United itacheza na Polisi Mara kwenye Uwanja wa Karume Mara wakati
Azam itacheza na Cosmopolitan kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Ndanda
itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Jumanne Januari 24, mwaka huu
Mtibwa Sugar itacheza na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa itacheza na JKT Ruvu huko Mafinga
huku Mbeya City ikipangwa kucheza na Kabela City Uwanja wa Sokoine mjini
Mbeya ilihali Madini na Panone zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid mjini Arusha.
Januari 25, mwaka huu kutakuwa na
mchezo kati ya Singida United na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Namfua
mjini Singida wakati mchezo mwingine utakaozikutanisha timu za African
Lyon na Mshikamano utapangiwa tarehe mpya. Mechi hiyo imepangwa
kufanyika Uwanja wa Uhuru.
..………………………………………………………………………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments :
Post a Comment