Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
11 Januari, 2017 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka
wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza watu
wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya
vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya
kuwahamasisha wananchi kufanya kazi
Dakta
Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa
Shule ya Msingi Somanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika
Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi hadi Bariadi
yenye urefu wa kilomita 71.8 iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90.
Amesema
kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara ambao wamekuwa
wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari
kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni
kutaka nchi iuze chakula nje ya nchi na sasa hao hao wanatangaza baa la
njaa.
''
Baadhi ya wanasisa walizungumza Bungeni kutaka wananchi waruhusiwe
kuuza chakula nje ya nchi kwa kuwa kuna chakula cha kutosha leo hii hao
hao wanatumia baadhi ya vyombo vya habari kutanga baa la njaa''
Akizungumzia
gharama za ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu, Rais Magufuli
ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu, Wizara ya Ujenzi na Wakala wa
majengo nchini TBA kukaa na kurejea gharama za ujenzi wa Hospitali hiyo
wa Shilingi Bilioni 46 kuwa hauendani na hali halisi ya aina ya jengo
linalotakiwa kujengwa.Rais Magufuli ametoa Shilingi bilioni 10 ili
kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo.
''Haiwezekani
majengo ya ghorofa ishirini lijengwe kwa shilingi Bilioni Kumi wakati
jengo la ghorofa moja moja lijengwe kwa gharama ya shilingi Bilioni 46''
Rais
Magufuli pia ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu kuendelea na ujenzi wa
mradi wa tenki la maji katika mlima Ngasamo ili wananchi wa mkoa wa
Simiyu ikiwemo wilaya ya Bariadi kupata huduma ya maji badala ya kukwama
kutokana na mwekezaji mmoja kutaka kuchimba madini ya Nikeli katika
mlima huo.
Amesema
haiwezekani wananchi zaidi ya milioni moja wakose maji kutokana na
mwekezaji mmoja ni kukosa muelekeo na kumkosea Mwenyezi Mungu kitu
kisichokubalika hivyo Waziri wa Nishati na Madini afute leseni ya
mwekezaji huyo ili wananchi wa Simiyu wapate huduma ya maji.
Rais
Magufuli amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania kwa ujumla
kutumia mvua chache zinazonyesha kulima mazao yanayostahamili ukame kama
vile Mtama,viazi na Uwele ili kuweza kujikimu kwa chakula badala ya
kutegemea chakula cha msaada kutoka Serikali.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Simiyu
11 Januari, 2017
0 comments :
Post a Comment