Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 9
Januari, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi
Chato,ambapo ndipo aliposoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na
kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Rais
Dkt Magufuli ameahidi kujenga madarasa matatu na ofisi moja ya walimu
katika Shule hiyo kufuatia ombi la Walimu kuwa shule hiyo inakabiliwa na
uhaba wa vyumba vya madarasa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi
wanaosoma shuleni hapo.
Aidha
Dkt.Magufuli amewaasa wanafunzi kutilia mkazo masomo ili waweze kufaulu
na kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia vyema fedha zinazotolewa na
Serikali kila mwezi katika kutoa elimu bila malipo na pasiwe na
wanafunzi hewa kama ilivyo kwa baadhi ya shule ambazo zimegundulika kuwa
na wanafunzi hewa katika uhakiki uliofanywa na serikali.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chato, Bwana Mwita Chacha
amemshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa msaada aliowapatia katika kukabiliana
na uhaba wa madarasa uliokuwa unaikumba shule hiyo, pia kuitembelea
Shule yao jambo ambalo limewatia moyo walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Rais
Magufuli pia ametembelea eneo la Stand ya zamani na kuzungumza na
baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo hilo na kutoa msaada kwa kikundi cha
wasafisha viatu ili kuongeza mtaji wa biashara yao.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
9 Januari, 2017
0 comments :
Post a Comment