Yahya
Jammeh ambaye amekua madarakani na kuingoza Gambia kama Rais kwa miaka
22 hatimae amekubali kuachia madaraka hayo na sasa Adama Barrow
aliyetangazwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu ndio anatarajiwa kuchukua
nafasi.
Kupitia
Television ya taifa, Yahya ametangaza kuachia madaraka ambapo AlJAZEERA
wameripoti kwamba taarifa kutoka IKULU zilisema baada ya kuachia
madaraka alitarajiwa kuondoka kwenye nchi hiyo ndani ya siku 3 ila media
nyingine zinasema amepewa saa tu za kuondoka.
TV
ya habari Nigeria imesema ECOWAS walimpa hadi saa sita mchana kuondoka
lakini mwenyewe akaomba muda huo usogezwe hadi saa kumi jioni na
imeripotiwa atakwenda kuishi Guinea.
Barrow
aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kusema ‘Yahya
Jammeh amekubali kuachia madaraka na anatarajiwa kuondoka kwenye nchi ya
Gambia leo’
0 comments :
Post a Comment