Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya FIFA
Ronaldo, 31, amewapiku Lionel
Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika
sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Ronaldo pia alishinda tuzo ya
Ballon d’Or mwezi Disemba mwaka jana, kufuatia mafanikio yake katika
Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016 akiwa
na timu ya taifa ya Ureno.
Meneja wa Leicester City Claudio
Ranieri ametajwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, huku
Silvia Neid, meneja wa zamani wa Ujerumani, akishinda kwa upande wa
wanawake.
0 comments :
Post a Comment