Waziri Mkuu wa Israel
Benjamin Netanyahu amesema amepokea mwaliko kutoka kwa Rais wa Marekani
Donald Trump kumuhitaji aende nchini Marekani mwezi ujao ili waweze
kujadiliana kuhusiana na uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini Israel,Netanyahu amesema mwaliko huo ni muhimu kwake kwani anatumai utaweza kumsaidia kupata ushauri ya nini kifanyike ili eneo la Mashariki ya kati liwe na amani.
Mkutano huo baina ya Trump na Netanyahu unakuja siku chache baada ya baadhi ya viongozi wakuu wa nchini Israel kuidhinisha ujenzi wa nyumba 560 kwa ajili ya walowezi, mashariki mwa Jerusalem.
Ujenzi huo kwa namna moja ama nyingine unadaiwa utachochea uhasama uliopo hivi sasa baina ya Waisraeli na Wapalestina ambapo Wapalestina wanatumai kuwa Jerusalem Mashariki itakuwa mji mkuu wa taifa lao litakapoundwa siku zijazo.
0 comments :
Post a Comment