Breaking Newzzz:Mbowe ,Gwajima, Manji Watajwa Na Makonda Awamu Ya Pili Sakata La Madawa Ya Kulevya


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo ameingia awamu ya pili ya kupambana na madawa ya kulevya na ametaja watu wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya kwa namna moja ama nyingine. 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Mchungaji Gwajima ni miongoni wa watu waliotajwa katika tuhuma za madawa ya kulevya na wamehitajika kufika central polisi siku ya Ijumaaa

Makonda: Awamu ya pili ya kupambana na madawa ya kulevya tumeianza leo.

Makonda: Nina orodha ya watu wengine ambao wanatakiwa kuripoti polisi siku ya Ijumaa

Makonda: Tutapita nyumba kwa nyumba, kila nyumba inayohisiwa, tutaingia, nawashukuru wenyeviti wa mitaa

Makonda: Hii vita tukishindwa, tumeshindwa wote, kuna watu wamekaa wanafikiri Makonda atashindwa

Makonda: Leo nina majina 65, juzi ile walikuwa kumi na kitu, mtasikia mtikisiko kidogo. Nataka tukutane nao.

Makonda: Wa kwanza ni mmiliki wa Slip Way, wenye klabu ya Yatch Klabu, Salehe wa MMI, Mwinyi Machapta

Makonda:Kuna dada yangu anaitwa Rose yuko China, kuna Mzee wangu anaitwa Kiboko anaishi Mbezi

Makonda: Kila tunayemuita ajue tunamfahamu kuliko anavyofikiri. Kuna mtu anaitwa Hafidh anaishi Mbezi Mwisho

Makonda: Kuna kaka yangu mpendwa mbunge mstaafu, Idd Azzan, naye namuhitaji

Makonda: Kuna kaka yangu Aikael Mbowe Mbunge wa hai ambaye ni mkazi wa DSM, kuna Bossi Kizenga wa Bunju

Makonda: Nassoro Selem wa Mabibo, kuna ndugu yangu Hussein Pamba Kali, pamoja na Mchungaji Gwajima

Makonda: Pamoja na kaka yangu Yusuph Manji pia namuhitaji, Mmiliki wa Sea Clif pia namuhitaji

Makonda: Makapuni matatu ya meli ambayo ni pamoja na Tanga Petrolium Ltd, GBP Tanzania Limited

Makonda: Kwenye zile nyumba ambazo wananchi mnazitilia shaka, toeni taarifa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment