Chama cha Wananchi (CUF) Kambi ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad
kimesema kinakwenda Mahakama ya Rufani kumpinga Jaji Sekieti Kihiyo
baada ya kugoma kujitoa kwenye kesi yao.
Kesi hiyo imefunguliwa na sehemu ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa
chama hicho, wanaoungwa mkono na Maalim Seif dhidi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa na Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na msajili,
Profesa Ibrahim Lipumba.
Wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama
hicho, ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya na wanachama
wengine tisa waliosimamishwa uanachama. Mwingine ni Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Katika kesi hiyo namba 23 ya mwaka 2016, bodi ya wadhamini CUF inaiomba
mahakama itoe amri ya kubatilisha barua ya Msajili inayomtambua Profesa
Lipumba kuwa ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CUF.
CUF iliwasilisha maombi ikimtaka Jaji Kihiyo ajitoe kusikiliza kesi hiyo
Desemba 6 mwaka jana, licha ya mambo mengine ikidai haina imani naye.
Katika uamuzi wa Desemba 14 mwaka jana, Jaji Kihiyo aligoma kujitoa
katika kesi hiyo akidai kuwa sababu zao hazina msingi na wadai
wanachokifanya ni kumtafuta jaji wanayemtaka wao.



0 comments :
Post a Comment