Mshauri mkuu wa baraza la usalama la taifa la Marekani, amerudishwa
kwenye kazi yake ya awali baada ya kukosoa sera za utawala wa Donald
Trump zinazohusiana na Latin America.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders, amesema Craig Deare
ameondolewa kwenye nafasi hiyo. Deare alidaiwa kuponda jinsi uongozi wa
Trump unavyoshughulika na masuala ya Latin America alipokuwa akizungumza
huko Washington.
Hii si mara ya kwanza kiongozi wa juu anatumuliwa kwa kumkosoa Trump.



0 comments :
Post a Comment