KOCHA WA STAND UNITED AFUNGIWA MECHI TATU


MORTO Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72), imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000 (laki tano).
Katika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu za JKT Ruvu na Stand United iliyochezwa Januari 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Morocco aliondolewa kwenye benchi (Ordered off) kwa kosa la kupiga maamuzi ya mwamuzi na kutoa lugha chafu.
Kamati hiyo ya Saa 72 imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 40 (11) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Makocha. Morocco hata kama atakuwa amemaliza mechi tatu nje ya benchi, hataruhusiwa kukaa kwenye benchi hadi awe amelipa faini hiyo.
Adhabu hiyo ya Morocco itaendelea kumhusu hata kama utakuwa umehamia kwenye timu nyingine na katika msimu mwingine wowote.

..………………………………………………………………………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment