Raundi ya Sita ya mechi za kuwania
Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup –
2016/17, itaanza Februari 24, 2017 kwa michezo minne kuchezwa kwa siku
hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaopigwa saa 1.00
jioni.
Michezo hiyo kwa mujibu wa ratiba
inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni
kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza
Stand United ya Shinyanga Uwanja wa kaitaba mjini Bukoba.
Mechi nyingine itakuwa ni kati ya
The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar
watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.
Jumapili Februari 26, mwaka huu
timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za
Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Jumatano Machi 1, 2017 Simba SC
itacheza na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam
wakati Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.


0 comments :
Post a Comment