Timu
ya Manchester City imepanda hadi katika nafasi ya pili katika msimamo
wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupambana na kuibuka na ushindi wa
magoli 2-0 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Vitality.
Akiwa
ameanzia benchi mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero,
aliingia katika dakika ya 14, kufuatia kuumia kwa mshambuliaji
anayemyima namba kwa hivi sasa Mbrazili Gabriel Jesus.
Lakini
alikuwa Raheem aliyeipatia Manchester City goli la kwanza, baada ya
kipa Artur Boruc kuokoa mara mbili magoli, Tyrone Mings alijikuta
akijifunga goli la pili kufuatia shinikizo la lililochangiwa na Aguero.
0 comments :
Post a Comment