WINGA wa Yanga, Simon Msuva, amesema katika maisha yake ya soka
hatasahau mwaka 2015 alivyozomewa na mashabiki wa klabu yake hiyo baada
ya kukosa penalti dhidi ya Simba, ambapo walifunga bao 1-0 mpaka akajuta
kuichezea timu hiyo lakini sasa mambo yako poa.
Msuva ambaye kwa sasa ana mabao 10 akiongoza kwenye msimamo wa
wafungaji, alisema baada ya kukosa penalti hiyo mashabiki walishindwa
kuvumilia wakaanza kumrushia maneno mazito huku wengine wakifikia hatua
ya kumtaka aondoke.
“Maisha ya mpira wa miguu hasa unapochezea hizi timu mbili za Simba na
Yanga yanataka uvumilivu sana, kwani bila hivyo unaweza ukaamua kuondoka
kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na maneno makali.
“Nakumbuka msimu wa mwaka 2015 ilitokea penalti upande wetu nikachukua
uamuzi wa kuipiga, lakini bahati mbaya sikufanikiwa kufunga nikatukanwa
sana mpaka nikajua, mchezo huo ulimalizika kwa sisi kupoteza tukifungwa
bao 1-0,” alisema.
Anasema tangu kukosa penalti hiyo alikosa raha kwani mashabiki walikuwa
wakimzomea sana huku wengine wakiutaka uongozi kutomwongezea mkataba
mpya, lakini hata hivyo alijipa moyo na yote hayo yakapita.



0 comments :
Post a Comment