Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea
kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali
ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi
na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na
wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa
matukio makubwa ya uhalifu.
Aidha Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na
wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha
mkoa wetu unakua mahala salama. Hata hivyo kumekuwa na tukio moja la
ajali ya kifo na majeruhi kama ifuatavyo :-
- AJALI YA KIFO NA MAJERUHI.
Tarehe 06.02.2017 saa 20:45hrs eneo
Inyala – Mablock, kata ya Inyala, tarafa ya Tembela, wilaya ya kipolisi
Mbalizi, mkoa wa Mbeya. Gari T.688 DHE aina ya Yutong basi mali ya
kampuni ya Super Feo ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbinga mkoa wa
Ruvuma, ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la ABDALLAH
MWINYIHERI, iliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo cha abiria
mmoja ambaye bado kutambuliwa, jinsi ya kiume, miaka kati ya 32 hadi 35
na majeruhi kwa ANNA MUHEZA [39], mkazi wa Mbeya na ANNA BRUNO [20],
mwanafunzi chuo kikuu cha Mzumbe – Mbeya ambao wamelazwa hospitali ya
rufaa Mbeya. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi, dereva alikimbia baada ya
ajali. Jitihada za kumtafuta zinaendelea.
Aidha kuna mafanikio yaliyopatikana katika misako ni kama ifuatavyo:-
- KUPATIKANA NA UNGA UDHANIWAO KUWA NI DAWA ZA KULEVYA.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
linamshikilia ANITHA ABEL [21], mwanafunzi kidato cha tatu wa shule
ya sekondari Sanani iliyopo [W] Mbozi [M] Songwe akiwa na kete 15 za
unga udhaniwao kuwa ni dawa za kulevya.
Tukio hilo limetokea tarehe
30.01.2017 majira ya saa 12:00hrs katika mtaa wa Mshikamano, kata ya
Nsalala, tarafa ya Usongwe, wilaya ya kipolisi Mbalizi, mkoa wa Mbeya.
Mtuhumiwa alikutwa katika harakati za kuuzia wateja dawa hizo na
alipoona Polisi alikimbilia chooni ambapo hata hivyo alikamatwa.
Taratibu za kisheria zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
- KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
linawashikilia wafanyabiashara nane wakazi wa jijini Mbeya kwa
kupatikana na mali ya wizi, vitenge jumla ya doti 1,075 kufuatia tukio
la wizi lililofanyika jijini Dar es salaam.
Tukio hili limetokea tarehe
06.02.2017 kati ya saa 11:00hrs hadi saa 15:00hrs eneo la
Mwanjelwa sokoni, kata ya Manga, tarafa ya Iyunga jijini Mbeya.
Watuhumiwa waliokamatwa na idadi ya doti za vitenge
kwenye mabano ni DENIS CHAULA [ doti 168], SALOME MGAYA
[doti 102], MAHOMI SANGA MWAKYOSA [doti 104], SUPE KANYAMALE
[doti 66], JANE MAHELA [doti 62], MATRIDA
NGAILO [doti 171], TUKAE MAJIO [doti 163] na JULIANA MAHENGE
[doti 239].
- KUINGIA NCHINI BILA KIBALI NA KUSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
linawashikilia raia 7 wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali
na pia wamekamatwa wasafirishaji watanzania wanne.
Tukio hili limetokea tarehe 31.01.2017
saa 02:40hrs kijiji cha Mpakani, kata ya Igawa, tarafa ya Rujewa,
wilaya ya Mbarali, mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa hao ni [1]. SUJUMI
PARACHO [40], [2] ELIAS HAVALA [22]. [3] GETSO TAVALA [25], [4].
TAMASKE LARE, [22], [5]. ZULFU MANGU [27], [6]. DABAVA LAFIVU [30],
na [7] SHETO HERISO [25], wote raia wa Ethiopia.
Katika tukio hilo wasafirishaji wa
wawahamiaji haramu hao ambao ni watanzania wanne walikamatwa wakitumia
gari T.347 DAJ aina ya Toyota Caravan haice. Watuhumiwa hao ni dereva
1. FILEX MLAGILA [32], 2. ELIAS S/O ARON [30], 3. FRED S/O PETER,
[23] na AZALIA S/O ELIAS, [30] wote wakazi wa Uyole
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu
Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa jamii
kuacha tabia ya kutumia dawa za kulevya kwani ni kinyume cha sheria na
ni hatari kwa afya ya mtumiaji. Aidha Kamanda Kidavashari anaendelea
kutoa wito kwa jamii kutoa taarifa juu ya mtu/ watu / kikundi au mtandao
wa wanaojihusisha na utumiaji, usafirishaji na uuzaji wa dawa za
kulevya ili hatua dhidi yao zichukuliwe mara moja.
Kadhalika Kamanda Kidavashari
anaendelea kutoa wito kwa jamii hususan watumiaji wa barabara na
madereva kuzingatia na kutii sheria za usalama barabarani ili kuepuka
ajali zinazoweza kuepukika. Pia ametoa wito kwa yeyote mwenye taarifa
juu ya mahali alipo dereva aliyesasababisha ajali na kukimbia azitoe
katika mamlaka husika ili akamatwe, vinginevyo ajisalimishe mara moja.
Imesainiwa na :
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


0 comments :
Post a Comment