Takwimu zilizompa tuzo ya mchezaji bora wa January wa VPL Juma Kaseja


Golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Kagera Sugar ya Bukoba Juma Kaseja ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi January wa Ligi Kuu Vodacom msimu wa 2016/2017.
Kaseja ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo aliyokuwa anawania na wachezaji wengine wawili, ambao ni Mbaraka Abeid anayecheza nae Kagera Sugar na Jamal Mtengeta anayeichezea Toto African ya Mwanza, Kaseja sasa atapewa zawadi ya Tsh milioni moja kutoka Vodacom.
Juma Kaseja
Kipa huyo ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Simba na Yanga kwa nyakati mbili tofauti na baadae kujiunga na Mbeya City kabla ya kujiunga na Kagera Sugar, takwimu zake za mwezi January zinaonesha kafungwa goli moja katika mechi zao tatu za January, huku timu yake ikifunga magoli 6.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment