VIDEO: Gari lililomundoa kituo cha Polisi Freeman Mbowe leo jioni



Leo mchana Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alifika kwenye kituo cha Polisi kati Dar es salaam kutii wito wa kuhojiwa na Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya baada ya jina lake kutajwa kwenye orodha February 8.
Baada ya kukaa kituoni hapo kwa zaidi ya dakika 60, Waandishi wa habari waliokua nje ya eneo hilo walishuhudia Mwenyekiti huyo akichukuliwa na Gari aina ya Land Cruiser iliyofatwa na magari mengine nyuma yake na kuelekea ambako Waandishi hawakufahamu mara moja.
Utaratibu huu wa kuwaondoa kituo cha Polisi kati ulifanyika pia kwa Askofu Gwajima na Mfanyabiashara Yusuph Manji ambapo baadae ilikuja kujulikana walipelekwa kwa Mkemia mkuu kupimwa kama wanahusika na utumiaji wa dawa za kulevya.
Endelea kukaa karibu na www.nkupamahmedia.com utaendelea kupata taarifa za kila kinachoendelea kwenye anga la Tanzania na nje ya Tanzania,
Video yenyewe ya gari lililomchukua Freeman Mbowe leo ndio hii hapa chini bonyeza play kuitazama
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment